Mkono wa kifo umeipokonya nchi yetu tukufu shujaa 14.
hapo jana mwendo wa saa tano asubuhi, ndege ya kijeshi (aina Y-12 ambayo imeundwa na kampuni ya uchina iitwao Harbin Aircraft Manufacturing Corporation)
iliokuwa ikiwasafirisha maafisa wa ngazi ya juu wa serikali paoja na viongozi wa eneo la magharibi mwa kenya, ilipata ajali.

Yamkini hali mbaya ya anga ilisababisha ajali hii kwani kulikuwa na mvua nyingi mno.
Viongozi hawa walikuwa safarini kueleka kwenye mkutano wa kuleta amani katika eneo hilo.
Hivi maajuzi kulikuwa kumezuka vita kati ya jamii tofauti zinazoishi huko magharibi kenya.
Walioaga dunia ni makamu kiongozi rasmi wa upinzani bungeni na pia mbunge wa eneo la North horr, daktari
Bonaya Godana. Pia alikuweko waziri msaidizi wa usalama wa taifa na pia mbunge wa eneo la Nakuru mjini,mheshimiwa
Mirugi kariuki aliyekuwa akiongoza ujumbe huo. Pia alikuweko waziri msaidizi wa maendeleo ya maeneo na pia mbunge wa laisamis, mheshimiwa
Titus Ngoyoni.

wengineo ni waheshimiwa
abdi sasura (mbunge wa saku),
guracha galgallo (mbunge wa moyale) na liuteni kanali mstaafu
abdulahi aden, wa bunge la afrika mashariki. Mkuu wa wilyaya ya moyale bwana
peter king'ola na pia mkuu wa polisi wa mkoa wa mashariki
bwana
thomas chigamba walifariki.Mchungaji
william wako wa kanisa la anglikana,meja
david macharia njoroge, kapteni
joseph njogu mureithi,
gibert siang'a katibu mdogo msaidizi ofisi ya rais, konstabu
yusuf nguyo na bwana
john ouma wa kitengo cha intelligence, pia waliaga dunia.
Kenya haijawahi kupata mkasa wa ajali aina hii ambao imeangamiza maafisa na viongozi wengi hivi.Ni huzuni kuwa wilaya za marsabit na moyale zimewapoteza wajumbe wao wote.
Vifo hivi pia vimeongeza jumla ya wabunge ambao wameaga dunia kufikia 13, tangu kikao hiki cha bunge ya tisa kuapishwa. Kwa kweli ni hofu kuu kwa rais wetu mtukufu
mheshimiwa Mwai Kibaki, pia kwa wananchi wa kenya na hata afrika mashariki kw ujumla.

Twaombea heri na baraka kwa walionusurika kifo.
kwa jamii za waliofariki, Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja wakati huu mgumu.
Kwa wananchi wa sehemu zote zilizoadhiriwa, poleni sana,
mimi nikiwa mmoja wao.( mbunge shujaa mirugi kariuki alikuwa ni kiongozi wa eneo nalotoka la nakuru mjini)
Pia kwa wakenya wote na hata afrika mashariki, tumshukuru Mola kwa baraka zake.
Mwisho ningependa kuzisihi jamii za eneo la magharibi mwa kenya kukumbatia amani
na uwiano ili msiba huu usiwe mtupu.
MUNGU AIBARIKI KENYA....