shukrani
nawashukuru nyote mlioniandikia wiki iliopita.Mshairi ameniuliza ni kwa nini jina la blogu ni "mhujumu wa sanaa zetu".
Maana ya jina hili ni kwamba ni vizuri kuwajulisha wanaotembelea blogu kuwa kile watsoma hapa ni sanaa tamthilia mila na desturi zetu waafrika na hasaa wale wanaoelewa kiswahili. kimombo nakielewa lakini ni vizuri sisi kama waafrika kuwasiliana kwa lugha ambayo mbeberu hatoelewa.
ningependa kumshukuru pia ndesanjo kwa kuimulika blogu hii.
kwa sasa mimi husoma blogu za ndugu zetu waliyo dayaspora na kuashiria mienendo ambayo yaweza kuwapotosha hasa wakiwa ng'ambo. Kwa mfano nimeweza kusoma blogu nyingi za kina dada zetu na kwa kweli kutokana na wanayoandika, inakaa kana kwamba hawafuati mila na desturi zetu. Si eti nawaingilia lakini sioni ni nini cha maana kwa dada akiashiria eti kwamba yeye anaufurahia upweke wake na kwamba hana shida na hali hiyo. pia kina ndugu zetu wengine wao wanaandika kuhusu vile wanavojihusisha na tabia za kupotosha na za makafeli. kw hiyo nawaomba tuzidi kulinda mila na desturi zetu. Wanasanaa wetu pia na wanasarakasi na wale wanapend tamthilia ni muhimu wajitokeze ili kuulinda mwenendo halisi wa wanaafrika.
mwisho .


2 Comments:
Karibu sana ndugu yetu Muhujumu (jina lako linanipa kigugumizi kidogo). Nafurahi kujua umetambua kuwa wakati umewadia sasa wa walau kuandika masuala ambayo beberu hataweza kuelewa. Akija kuelewa tutakuwa tumepiga hatua nuyingine kabisa.
Hongera kwako.
Post a Comment
<< Home