uhujumu!!!

Thursday, March 09, 2006

homa ya bird flu

hivi majuzi, kumetokea vifo vya ndege kadhaa humu nchini. serikali kupitia wizara zake imefanya uchunguzi wake na kuthibitisha kuwa homa hii ya bird flu haimo nchini.
lakini kutokana na vifo hivi ambavyo vimetokea sehemu kadha nchini, nafikiri kwamba
serikali inaficha ukweli, kisa na maana, hatujui.
homa hii ilifika kwanza Nigeria na kisha kuenea hadi Ethiopia. kwa sasa kulingana na mienendo ya ndege wa pori wanaosafiri, kenya haimo kwenye matata. lakini ndege hawa katika hali yao ya kusafiri kaskazini mwa afrika, kuna uwezekano kuwa walikutana na ndege wengine humu nchini na kuwaambukiza. juzi hapa nairobi, ndege wakubwa waitwao marabou stocks wamefariki na kuanguka kutoka kwa makao yao mitini, bila ya yeyote kuwachokoza!!!! hii inaonyesha kuwa kunauwezekano wa homa hii kuwa nchini!!!
lakini kama kawaida, serikali ilikataa na ilipochunguza, iliazimia kuwa ni homa aina ya newcastle.
ole wetu wakenya kama ukweli umefichwa!!!

2 Comments:

At 9:33 PM, Blogger shyneone said...

Naelewana nawe ndugu. Kunaufichaji kabisa, bila shaka.
Lakini kisa na hali, ya kutojulisha wananchii ni nini?
Hii serikali yetu ina mambo tele!
ajaba ya kwamba vifo vya watu zikianza, ndivyo tutapashwa habari hii.
Je tufanyeje kujulisha hii serikali kwamba ugonjwa huu ni hatari na waeza kuenea kama moto usipochunguzwa?
Nina Hasira nyingi kwenye hii tatizo, kwa hivyo serikali uwache upumbavu. Maisha ya wnadamu ni muhumi.

 
At 10:06 AM, Blogger akiey said...

Tusije tukawa kama Uchina wakati janga la Ukimwi lilipokuwa linaenea na serikali yao ikawa inahadaa raia wake na ulimwengu kwa jumla kuhusu kasi ya kuambukizika Wachina...ama tukawa kama serikali ya Urusi pale Kursk, ile meli yao ya kivita ya chini ya bahari (submarine) ilipozama na kuhatarisha maisha pamoja na kusababisha vifo vya wanamaji wao.

Raia wana haki ya kufahamishwa mapema ili tuweze kuchukua hatua barabara za kujikinga na maradhi haya.

 

Post a Comment

<< Home