uhujumu!!!

Wednesday, March 01, 2006

tatizo la ukabila

ukabila ni nini?? hili ni swali ambalo limeleta jinamizi na mtafaruko kati yetu wakenya. Nafikiri ukweli wa mambo ni kuwa ukabila umetokana na siasa mbaya ambazo nchi yetu imesingizia kwa muda. ndugu zetu watanzania hawana shida ya ukabila pia wanauganda nafikiri hawana shida ya ukabila.
wakenya wamepotozwo na viongozi wao wa kisiasa na kusingiziwa kuwa kuna mvutano kati ya kabila za wakenya. suluhisho ni kutumia lugha moja haswa kiswahili ambayo wakenya kwa ujumla wanijua. pia ni wakati wa vijana kuuchukua mwongozo wa nchi hii tukufu.
wakenya mara kwa mara huelezwa kuwa ni wakati wa kundi au kabila fulani "kula".
huu ni upotofu ambao unastahili kukemea kwa hima na dhati!!
sisi kama vijana tusizidi kudanganywa na kupotoshwo. Wakati wa uchaguzi inafaa tuwateuwe viongozi wanaoashiria mipango ya maendeleo nchini na wala si wale ambao wantumia ukabila kama ngao yao. Kwa kweli ni huzuni kuelezwa kuwa vijana hawataweza kujiandikisha kama wapigaji kura kwa muda wa miezi sita kwa sababu hawataweza kupata vitambulisho!! huu ni msiba na pia ufisadi. ni kwa nini serikali ilipeana kandarasi ovyo kwa kampuni ambayo haitoweza kukamilisha kazi ya kutayarisha fomu za kusajili wanachi???
lakini ni vema kujua bado kuna mda. Mwaka ujao kwa mjalio. nawasihi vijana kujiandikisha kwa wingi ili tuing'atue mwongozo huu wa wazee ambao wanpotosho nchi.
watanzani walipiga kauli moja na kumchagua rais shupavu na ambaye anayaelewa mahitaji ya vijana. Waganda pia waliazimia kuuendeleza mwongozo wa rais museveni ambaye kwa maono yangu, anayaelewa mahitaji ya vijana.
Hivo basi ni jukumu la sisi vijana wa kenya kukataa ukabila na shinikizo la viongozi waliopo sasa. ( namaanisha wote wa milengo yote...KANU, LDP , NAK, DP .FORD...na kadhalika. )
wakati ni wetu vijana.

2 Comments:

At 9:58 PM, Blogger shyneone said...

This comment has been removed by a blog administrator.

 
At 2:46 AM, Anonymous mtandawazi said...

Umegota ndipo mtaalamu mwenza. Kando na kuifanya lugha ya kiswahili kuwa lugha ya kila mkenya, itabidi hii iwe sera inayoungwa mkono kutoka ngazi za juu serikalini. Kwa mfano wazazi watakaowakuza watoto wao kwa lugha na desturi ya Kiswahili watuzwe. Wazazi watakaowapa watoto wao majina yasiyojiegemeza kwa kabila lao watuzwe pia. Wabunge watakaojieleza kwa ufasaha kwa lugha ya Kiswahili bungeni watunukiwe zawadi n.k. Nikidhani juhudi kama hizi zitapelekea kupunguza ukabila.

 

Post a Comment

<< Home