uhujumu!!!

Tuesday, April 11, 2006

KENYA YAPOTEZA SHUJAA...


Mkono wa kifo umeipokonya nchi yetu tukufu shujaa 14.

hapo jana mwendo wa saa tano asubuhi, ndege ya kijeshi (aina Y-12 ambayo imeundwa na kampuni ya uchina iitwao Harbin Aircraft Manufacturing Corporation)
iliokuwa ikiwasafirisha maafisa wa ngazi ya juu wa serikali paoja na viongozi wa eneo la magharibi mwa kenya, ilipata ajali.

Yamkini hali mbaya ya anga ilisababisha ajali hii kwani kulikuwa na mvua nyingi mno.
Viongozi hawa walikuwa safarini kueleka kwenye mkutano wa kuleta amani katika eneo hilo.
Hivi maajuzi kulikuwa kumezuka vita kati ya jamii tofauti zinazoishi huko magharibi kenya.

Walioaga dunia ni makamu kiongozi rasmi wa upinzani bungeni na pia mbunge wa eneo la North horr, daktari Bonaya Godana. Pia alikuweko waziri msaidizi wa usalama wa taifa na pia mbunge wa eneo la Nakuru mjini,mheshimiwa Mirugi kariuki aliyekuwa akiongoza ujumbe huo. Pia alikuweko waziri msaidizi wa maendeleo ya maeneo na pia mbunge wa laisamis, mheshimiwa Titus Ngoyoni.

wengineo ni waheshimiwa abdi sasura (mbunge wa saku), guracha galgallo (mbunge wa moyale) na liuteni kanali mstaafu abdulahi aden, wa bunge la afrika mashariki. Mkuu wa wilyaya ya moyale bwana peter king'ola na pia mkuu wa polisi wa mkoa wa mashariki
bwana thomas chigamba walifariki.Mchungaji william wako wa kanisa la anglikana,meja david macharia njoroge, kapteni joseph njogu mureithi,
gibert siang'a katibu mdogo msaidizi ofisi ya rais, konstabu yusuf nguyo na bwana john ouma wa kitengo cha intelligence, pia waliaga dunia.

Kenya haijawahi kupata mkasa wa ajali aina hii ambao imeangamiza maafisa na viongozi wengi hivi.Ni huzuni kuwa wilaya za marsabit na moyale zimewapoteza wajumbe wao wote.
Vifo hivi pia vimeongeza jumla ya wabunge ambao wameaga dunia kufikia 13, tangu kikao hiki cha bunge ya tisa kuapishwa. Kwa kweli ni hofu kuu kwa rais wetu mtukufu mheshimiwa Mwai Kibaki, pia kwa wananchi wa kenya na hata afrika mashariki kw ujumla.

Twaombea heri na baraka kwa walionusurika kifo.
kwa jamii za waliofariki, Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja wakati huu mgumu.
Kwa wananchi wa sehemu zote zilizoadhiriwa, poleni sana, mimi nikiwa mmoja wao.( mbunge shujaa mirugi kariuki alikuwa ni kiongozi wa eneo nalotoka la nakuru mjini)

Pia kwa wakenya wote na hata afrika mashariki, tumshukuru Mola kwa baraka zake.
Mwisho ningependa kuzisihi jamii za eneo la magharibi mwa kenya kukumbatia amani
na uwiano ili msiba huu usiwe mtupu.





MUNGU AIBARIKI KENYA....

1 Comments:

At 8:19 AM, Blogger kritik said...

maombi yetu kwa mola awafariji jamii za waliotuacha.
ehh mhujumu, your swa is timam!!
keep it up sleuth...

 

Post a Comment

<< Home