uhujumu!!!

Wednesday, April 26, 2006

mswada dhidi ya unajisi na hatia za ngono.

Mbunge maalum bi. Njoki Ndungu atiweka rekodi kwa kuwa mbunge wa pili tu

aliyewasilisha mswada wa kibinafsi bungeni. wakwanza alikuwa ni marehemu j.m kariuki,

aliyewasilisha mswada wa "hire purchase"

Mswada wa Njoki unakisia kuwaadhibu wanaoendeleza maovu ya kunajisi wanawake

na haswa watoto.

Ni jukumu la wabunge kuupitisha mswada huu muhimu ili tatizo hili

liweze kupata suluhisho.

Wednesday, April 19, 2006

serikali yaidhinisha ijumaa 21 aprili. kama sikukuu ya maombi


Kutokana na msiba ulijiri nchini wiki iliopita, serikali imetenga siku ya ijumaa tarehe 21 aprili
kama siku ya maombi.
Rais wetu mtukufu, Mwai Kibaki ataliongoza taifa katika ibaada ya maombi ya makanisa yote.
Ibaada hii itakuwepo hapo KICC mwendo wa saa saba adhuhuri.
Hivo basi serikali imeitenga siku hiyo kama sikukuu maalum ili kuwezesha wakenya wengi kuhudhuria ibaada hiyo.
Pia kutakuwa na maombi kama haya katika viti vyote vya serikali vya mikoa, wilaya na hata tarafa zote nchini.
Sote tujitolee tufike ili tuweze kumrudishia mola sifa zake na pia kuombea nchi yetu tukufu.
ripoti hii imechapishwa kwenye mtandao wa msemaji rasmi wa serikali

Thursday, April 13, 2006

tuzo za KBW-2006

Yamkini mashabiki wa toleo hili la Uhujumu wameamua
kuliteua kama mojawapo ya zile blogu ambazo wanaKBW
watazipigia kura.
Nawashukuru nyote ambao mmefurahia uhujumu na pia
kwa wale ambao ni mara ya kwanza kuitembelea uhujumu.

Mimi kama mhujumu, nitazidi kuangazia mambo ambayo
yanaadhiri mila desturi na mienenendo yetu sis waafrika.
Natumai kwamba mtaipigia uhujumu kura kama
"blogu inayopendeza isiyo ya kimombo, ama ukipenda, kiingereza."

Nanyi wanaKBW nawasihi mpige kura kwa wingi.
Ni haki yako kama MwanaKBW kupiga kura yako.

Na kwa wale wengine ambao wameteuliwa, nawapa
hongera na kuwatakia mema.

Kwa mara ingine, shukrani, na pigia uhujumu kura

Tuesday, April 11, 2006

KENYA YAPOTEZA SHUJAA...


Mkono wa kifo umeipokonya nchi yetu tukufu shujaa 14.

hapo jana mwendo wa saa tano asubuhi, ndege ya kijeshi (aina Y-12 ambayo imeundwa na kampuni ya uchina iitwao Harbin Aircraft Manufacturing Corporation)
iliokuwa ikiwasafirisha maafisa wa ngazi ya juu wa serikali paoja na viongozi wa eneo la magharibi mwa kenya, ilipata ajali.

Yamkini hali mbaya ya anga ilisababisha ajali hii kwani kulikuwa na mvua nyingi mno.
Viongozi hawa walikuwa safarini kueleka kwenye mkutano wa kuleta amani katika eneo hilo.
Hivi maajuzi kulikuwa kumezuka vita kati ya jamii tofauti zinazoishi huko magharibi kenya.

Walioaga dunia ni makamu kiongozi rasmi wa upinzani bungeni na pia mbunge wa eneo la North horr, daktari Bonaya Godana. Pia alikuweko waziri msaidizi wa usalama wa taifa na pia mbunge wa eneo la Nakuru mjini,mheshimiwa Mirugi kariuki aliyekuwa akiongoza ujumbe huo. Pia alikuweko waziri msaidizi wa maendeleo ya maeneo na pia mbunge wa laisamis, mheshimiwa Titus Ngoyoni.

wengineo ni waheshimiwa abdi sasura (mbunge wa saku), guracha galgallo (mbunge wa moyale) na liuteni kanali mstaafu abdulahi aden, wa bunge la afrika mashariki. Mkuu wa wilyaya ya moyale bwana peter king'ola na pia mkuu wa polisi wa mkoa wa mashariki
bwana thomas chigamba walifariki.Mchungaji william wako wa kanisa la anglikana,meja david macharia njoroge, kapteni joseph njogu mureithi,
gibert siang'a katibu mdogo msaidizi ofisi ya rais, konstabu yusuf nguyo na bwana john ouma wa kitengo cha intelligence, pia waliaga dunia.

Kenya haijawahi kupata mkasa wa ajali aina hii ambao imeangamiza maafisa na viongozi wengi hivi.Ni huzuni kuwa wilaya za marsabit na moyale zimewapoteza wajumbe wao wote.
Vifo hivi pia vimeongeza jumla ya wabunge ambao wameaga dunia kufikia 13, tangu kikao hiki cha bunge ya tisa kuapishwa. Kwa kweli ni hofu kuu kwa rais wetu mtukufu mheshimiwa Mwai Kibaki, pia kwa wananchi wa kenya na hata afrika mashariki kw ujumla.

Twaombea heri na baraka kwa walionusurika kifo.
kwa jamii za waliofariki, Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja wakati huu mgumu.
Kwa wananchi wa sehemu zote zilizoadhiriwa, poleni sana, mimi nikiwa mmoja wao.( mbunge shujaa mirugi kariuki alikuwa ni kiongozi wa eneo nalotoka la nakuru mjini)

Pia kwa wakenya wote na hata afrika mashariki, tumshukuru Mola kwa baraka zake.
Mwisho ningependa kuzisihi jamii za eneo la magharibi mwa kenya kukumbatia amani
na uwiano ili msiba huu usiwe mtupu.

MUNGU AIBARIKI KENYA....